CHOKORAA NA KALALA Jr MAMBO SAFI TWANGA PEPETA …Mapande na Maga nao wasamehewa


HATIMAYE Twanga Pepeta imemalizana kiroho safi na waimbaji Khalid Chokoraa na Kalala Jr ambao wanaendelea kuitumikia bendi hiyo kama kawaida.

Wiki iliyopita mkurugenzi wa Twanga Pepeta alicharuka na kuwatimua kazi Rogart Hegga ‘Katapila’ na Ferguson kwa kujianzishia bendi yao (DSS Band) kinyemela.

Aidha, Asha Baraka pia aliwatimua wanenguaji wa kiume Mapande na Maga kwa kuhusishwa na DSS Band, lakini baadae madansa hao wakasamehewa baada ya kuikana bendi mpya.

Ukungu ulitanda pia kwa Chokoraa na Kalala Jr ambao walituhumiwa kukataa kusafiri na bendi kwenda mkoani Ruvuma wakati wa X-Mas.

Asha Baraka akaweka wazi kuwa suala la Chokoraa na Kalala Jr litaamuliwa na menejimenti.


Mkurugenzi huo wa Twanga Pepeta ameiambia Saluti5 wiki hii kuwa Chokoraa na Kalala Jr ni safi na suala lao limekwisha baada ya menejiment kujiridhisha kuwa wasanii hao walipewa ruhusa. 
 Mapende akiwajibika kwenye jukwaa la Twanga Pepeta ndani ya Mango Garden Ijumaa iliyopita
Chokoraa kwenye jukwaa la Twanga Pepeta ndani ya Mango Garden Ijumaa iliyopita
 Kalala Jr na Chokoraa jukwaani na Twanga Pepeta kama kawa
 Kalala Jr akiimba na Twanga Pepeta Ijumaa iliyopita
Maga akiwajibika kwenye jukwaa la Twanga Pepeta ndani ya Mango Garden Ijumaa iliyopita baada ya kusamehewa

No comments