CHRISTIAN BELLA ASEMA KEJELI ZINGEKUWA ZINAKWAMISHA KIPAJI BASI ANGEKUWA AMEMALIZIKA SIKU NYINGI SANA


Mkali wa masauti Christian Bella amesema iwapo kejeli za wadau wa muziki zingekuwa zinamshusha msanii, basi yeye angekuwa amemalizika kisanii siku nyingi sana.

Bella amedai kwamba kwa muda mrefu amekuwa akipata shutuma zilizojaa kejeli kwa baadhi ya wadau wa muziki lakini daima amekuwa akizipuuza.

Akiongea na kipindi cha Afro TZ cha Radio One wiki iliyopita, Bella akafichua kuwa mara nyingi  amekuwa akiambiwa kuwa ana copy nyimbo za wasanii flani wa Congo kitu ambacho hakina ukweli wowote.

Aidha, Bella akasema shutuma nyingine ni hii ya kuambiwa hapigi dansi na badala yake anapiga bongo fleva.

“Mimi ni mwanamuziki wa dansi, lakini napiga muziki wa biashara, nasoma alama za nyakati kuangalia nini kinahitajika sokoni,” alifafanua Bella.

“Huwezi kubaki katika mapigo yale yake miaka nenda rudi, msanii ni lazima ubadilike ili soko lisikuache nyuma,” aliongeza Christian Bella.


No comments