CHRISTIAN BELLA KUWASHA MOTO TOROKA UJE TABATA JUMAMOSI HII


MFALME wa masauti Christian Bella, Jumamosi hii atawasha moto wa burudani kwa wakazi wa Tabata ndani ya ukumbi wa Toroka Uje.

Bella anatinga Toroka Uje kwa staili ya aina yake ambapo wakati bendi kibao zinazotumbuiza hapo zinapiga kwa mtindo wa ‘kiingilio kinywaji’, yeye onyesho lake hutaweza kulishuhudia bila kulipa shilingi elfu 10,000 mlangoni.

Onyesho hilo la Bella na kundi lake la Malaika Band, litakuwa maalum kwaajili ya kuwatambulishia wakazi wa Tabata wimbo wake wa “Nishike”.

No comments