CONTE AANZA MAZUNGUMZO NA MIROSLAV KLOSE KWA AJILI YA KUZIBA PENGO LA DIEGO COSTA "ANAYEMJAMBISHA"

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte anatambua tishio lililopo la kuondoka kwa mpachika mabao wake mahiri, Diego Costa na sasa anasaka mbadala wake.

Taarifa za ndani zinasema kuwa kocha huyo wa zamani wa Italia yumo katika mazungumzo na straika Miroslav Klose ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza kandarasi yake ya Lazio tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Imebainika kuwa kocha Antonio Conte anahitaji saini ya mfumania nyavu kwa ajili ya kuziba pengo la Diego Costa ambaye anatishia kutimkia kusakata soka katika klabu mojawapo ya nchini China.

Pamoja na Chelsea na Paris Saint-Germain, pia Genoa nao wameingia katika mbio hizi za kumwania mwanandinga huyo.

Klose alikuwa anatumika kama kiungo mshambuliaji katika kikosi cha Lazio katika Ligi ya msimu mzima uliopita.


“Klose kwa sasa ni mchezaji huru na kila kitu kinakwenda vyema kwa ajili ya kutua Chelsea. Kocha Antonio Conte yumo katika mazungumzo nae kwa muda mrefu,” kilinukuu chanzo cha habari ndani ya Stanford Bridge.

No comments