DARASA AHOFIA “MUZIKI” KUACHIA WIMBO MPYA

RAPA Darasa amesema kuwa kuendelea kukubalika kwa wimbo wake unaotamba uitwao “Muziki” kunampa hofu ya kuhitaji kufanya kitu kikubwa zaidi ya ngoma hiyo iliyopachikwa jina la utani la “wimbo wa taifa.”

“Video ya wimbo wangu huo imeshatazamwa zaidi ya mara milioni mbili kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa, hii inaonyesha kuwa “Muziki” ni wimbo mkali na ninatakiwa kuumiza kichwa zaidi ili baadae niibuke na mkali zaidi,” alisema.

Nyota huyo ambaye hivi karibuni alinusurika kwenye ajali ya gari dogo ambamo yeye na wenzake walitoka na majeraha madogo, amesisitiza kuwa wimbo wake huo haumfanyi kubweteka na badala yake unampa mizuka ya kutafuta mafanikio zaidi.


“Siku zote nimekuwa nikisema kuwa ninataka kufanya kitu ambacho hata nikipumzika muziki kitaendelea kutangaza jina langu, ndio maana siwezi kubweteka kwa sababu tu ya wimbo huu kuwa juu,” alisema.

No comments