DARASA AKANA KUMCHOKONOA DIAMOND PLATNUMZ KWENYE WIMBO "MUZIKI"

RAPA Darasa ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa “Muziki”, amesema kwa sasa hana mpango wa kutafuta “kiki” kwa kumchokoza msanii mwenzake kwa madai kwamba nyimbo zake zinajitosheleza kumbeba.

“Nimeamua kusema ukweli huu kwani kuna watu wanasema kuwa ule mstari wangu unaosema… sio samba sio chui sio mamba, nimemwimba Diamond ili kutafuta kiki, lakini ukweli ni kwamba nyimbo zangu zinajitosheleza kunibeba,” alisema darasa.

Alisema kuwa Diamond yuko juu kimuziki na ni zaidi ya simba na angeweza kujiita jina linguine kubwa kwavile ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Tanzania, lakini sio kwamba yeye anatafuta kiki kwake.


“Kwa hiyo niseme tu kwamba sijamshambulia Diamond katika wimbo wangu kwa lengo la kutafuta kiki, ila nimetoa ushauri kwake kwani ninatambua mchango wake katika muziki wa Kizazi Kipya,” alisema.

No comments