DARASA ASEMA KUFANIKIWA KWA WIMBO "MUZIKI" HAKUMFANYI AJISAHAU KUKAZA BUTI

RAPA nyota anayetamba na wimbo "Muziki", Darasa amesema mafanikio ya wimbo wake huo hayatamfanya alale bali ataendea kukomaa ili afanye vitu vikubwa zaidi ikiwemo kutoa albamu ambayo inaiandaa.

Darasa amepata mafankio ambayo hajawahi kuyapata baada ya wimbo "Muziki" kutazamwa zaidi ya mara mil 3.3 kwenye youtube katika kipindi cha chini ya miezi miwili tangu alipouachia Novemba 23.

Amesema, anataka mafanikio hayo yafuatie na albamu.


Amesema, anajua kuna baadhi ya wasani ambao wanadai hawaelewi ujumbe uliomo katika wimbo wake wa muziki na kufafanua kuwa ana muda wa kufanya kazi na siyo kushindana na watu.

No comments