DAVINA ASEMA NI NGUMU KUISHI KWA KUTEGEMEA FILAMU PEKEE

NYOTA wa Bongomuvi, Halima Yahya “Davina” anaamini kuwa ni ngumu kwa msanii kuishi kwa kutegemea filamu tu kwasababu soko hilo limeanguka sana nchini.

Badala yake Davina amewakumbusha wasanii wenzake wafanye shughuli mbalimbali zitakazowaletea maendeleo.

Alisema mambo yamebadilika sana hivi sasa na kwamba wale waliokuwa wamezoea maisha ya kuungaunga hawana nafasi tena.


Alisema kuwa fursa zipo nyingi za kuwawezesha wasanii kuwaongezea kipato kama yeye alivyoamua kujikita kwenye biashara za nguo na vitu mbalimbali ambavyo amekuwa akivifuata nje ya nchi na kuviuza.

No comments