DAYNA NYANGE ACHEKELEA VIDEO YAKE YA "KOMELA" KUTOKA POA

NYOTA wa muziki wa Kizazi Kipya, Mwanaid Said a.k.a “Dayna Nyange” amefurahishwa na ubora wa video ya wimbo wake wa “Komela” akisema inampa mzuka wa kufanya kazi nzuri zaidi.

Video hiyo aliyomshirikisha rapa Billnas imeruka hewani tayari na Dayna amesema ana furaha kuona kwamba imepata mapokezi mazuri.

“Watu wameisifia kuwa ni video nzuri name nakubaliana nao. Kwa sasa twende kwenye You Tube tuiangalie halafu baadae mtafurahi sana,” alisema.


Dayna alipata kutamba na nyimbo kama “Nivute Kwako” uliompaisha, “Nitulize” aliomshirikisha rapa Nay wa mitego, “Mafungu” aliomshirikisha Marlaw na “Sio Poa” alioimba na mshindi wa Bongo Star Serch II, Misoji Mkwabi.

No comments