MWIMBAJI wa muziki wa Kizazi Kipya, Dayna Nyange amesema kuwa hana mpango wa kumweka wazi mpenzi wake kwa vile hayo ni mambo yake binfsi na siyo lazima kila mtu kuyafahamu.

Alisema kuwa uhusiano wa kimapenzi mara nyingi huwa sio wa kudumu na kwamba mtu anaweza kumeka wazi mpenzi wake leo lakini akijikuta ksho mapenzi yamekufa, hivyo mtu mtu wa kumweka hadharani ni mume wake tu.

"Msimamo wangu katika maisha ni kwamba ninapenda kumweka hadharani mume wangu nitakayefunga nae ndoa na si mpenzi wa kawaida ambaye sio mtu wa kudumu," alisema.

Alisema, katika maisha msichana anayeweza kuwa na mtu ambaye anampenda sana lakini hawezi kujua upande wa pili kama mvulana huyo nae ana upendo wa aina hiyo.


Alisema kuwa katika mazingira hayo inamuwia vigumu kumweka hadharani mtu ambaye hana uhakika nae ndiyo maana haoni umuhimu kumweka wazi mtu wa kupita tu.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac