DEMU WA DELE ALLI AFUNIKA KWA UREMBO ENGLAND

WAKATI kiungo wa Tottenham Hotspur, Dele Alli ndio gumzo kwa sasa kwenye Ligi Kuu England, nae mchumba wake amewaacha mashabiki wa soka vinywa wazi.

Baada ya picha za demu huyo aitwaye Ruby Mae kuchapishwa kwenye vyombo vya habari vya Uingereza, mashabiki wa soka wa England wamempa alama kuwa ndie demu bomba zaidi miongoni mwa wachumba na wake wa nyota wanaocheza Ligi Kuu England.

Ruby ambaye ni mwanamitindo hivi karibuni aling’ara kwenye maonyesho ya mavazi jijini London.

Alli ambaye aliiua Chelsea kwa kufunga mabao mawili kwenye mechi baina ya timu hizo mbili nae alihudhuria onyesho hilo akiwa amevalia koti refu jeusi.


Wakati Alli akitamba kwenye Ligi Kuu England, mchumba wake Ruby nae anatikisa yakija masuala ya urembo.

No comments