DIAMOND PLATNUMZ ASEMA HUU SI WAKATI WA KUKATISHANA TAMAA …adai ameajiri vijana 40 ofisini kwake


MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amewataka watu walioponda kukabidhiwa kwake bendera ya taifa wakati akienda kutumbuiza michuano ya soka ya AFCON, wabadilike na wawe na moyo wa kizalendo.

Diamond amesema kwenda kwake Gabon kwenye AFCON ni matokeo ya jitihada zake za kuusongesha muziki wa Tanzania kwenye medani za kimataifa, hivyo ni hatua inayostahili kuungwa mkono.

Akiongea katika kipindi cha Sport Bar cha Clouds TV, Diamond alisema mara zote watu wamekuwa wakishutumu kuwa serikali haisapoti sanaa, lakini sasa tunaanza kuona tukiungwa mkono na serikali, lakini bado shutuma zinaendelea.

“Mimi nimeajiri vijana 40 ambao wako ofisini kwangu na napaswa kuwalipa kila mwezi, naumia sana kuona watu wanafanya juhudi za kutuvunja moyo,” alisema Diamond.

No comments