DIEGO COSTA AMALIZANA KIROHO SAFI NA ANTONIO CONTE ...arejea kikosini kuivaa Hull City


KOCHA wa Chelsea Antonio Conte na mshambuliaji wake Diego Costa wamemaliza mgogoro wao ulioibuka wiki iliyopita.

Costa aliibua mgogoro mazoezini kwa kusema anaumwa paja kitu ambacho Conte na jopo lake la madaktari wa Chelsea hawakukikubali.

Hatua hiyo ilimfanya Costa akose mchezo dhidi ya Leicester City, lakini sasa nyota huyo amemalizana na Conte na amerejea mazoezni tayari kwa mchezo dhidi ya Hull City Jumamosi hii.

Costa alipewa kibano cha kufanya mazoezi ya peke yake lakini hatimaye amejumuishwa na wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza.

No comments