DIEGO COSTA AMMIMINIA SIFA ANTONIO CONTE… asema ni kocha bora atakayeipa mafanikio klabu yao

STRAIKA wa kutumainiwa ndani ya kikosi cha Chelsea, Diego Costa amemmwagia sifa kocha wake, Antonio Conte na kumtaja kama ni kocha bora atakayeipa mafanikio klabu hiyo hata kutwaa ubingwa wa msimu huu.

Diego amenukuliwa akisema kuhusu Conte kuwa tangu achukue jukumu la kuinoa Chelsea ameifanya timu kurudi taratibu katika mstari wa kusaka ubingwa wa primier msimu huu.

“Ukiniuliza mimi ninaweza ninaweza kukwambia jambo moja kuwa Conte ni kocha bora kwasababu ameibadili timu tangu pale alipopewa jukumu.”

“Chelsea ya sasa ni tofauti na ile iliyokuwa chini ya makocha waliopita, kuna tofauti kubwa hata ya namna timu inavyocheza kwa wachezaji kushirikiana dimbani.”

“Tangu atue mwaka jana ameonyesha mambo ambayo sisi kama wachezaji tunaweza tukawa sehemu ya kuzungumzia mabadiliko haya,” alisisitiza Costa.


“Tunacheza tukiwa na furaha na imani kubwa chini yake kama atapewa muda zaidi wa kuendelea kuwa hapa nina imani kuwa kuna jambo linaweza kubadilika na hata timu kurejea katika kiwango cha soka la zamani.”

No comments