DIEGO COSTA APAGAWA NA MIFWEDHA YA WACHINA… agomea mazoezi na kukoromeana na kocha wake

MAMILIONI ya Ligi Kuu China yamemvuruga mfungaji tegemeo wa Chelsea, Diego Costa kiasi cha kugombana na kocha wake, Antonio Conte.

Klabu ya Tianjin Quanjin ya China inadaiwa kutenga dau la kiasi cha pauni mil 80 kwa ajili ya kumnasa costa na iko tayari kongeza mshahara wake na kuwa pauni 575,000 kwa wiki.

Wakala Jorge Mendez ambaye anamwakilisha Costa alikutana na tajiri wa klabu hiyo juzi.

Wakati haya yanatokea, Costa aligoma kufanya mazoezi juzi kwa kisingizio anaumwa mgongo.

Daktari wa klabu hiyo, PaoloBertelli alimpima nyota huyo na kudai alikuwa mzima wa afya.

Kitendo hicho kilimuudhi Conte na kumfanya kuzozana na mchezaji huyo.


“Haya nenda zako China bwana,” alisikika Conte akimwambia Costa kwa ukali wakati wakizozana.

No comments