DIEGO COSTA, SANCHEZ WAZIUMIZA KICHWA CHELSEA NA ARSENAL

KLABU za Arsenal na Chelsea zinakabiliwa na mtihani mzito wa kuwabakiza washambuliaji wake nyota; Alexis Sanchez na Diego Costa.

Sio siri katika kipindi cha miaka saba Ligi Kuu England imetawaliwa na washambuliaji kutoka bara la Amerika Kusini, sasa Arsenal na Chelasea ziko katika presha ya kuwabakiza nyota hawa wenye asili ya Latin Amerika.

Sanchez aliifungia Arsenal bao la ushindi dakika za jioni wakati walipoilaza Burnley mabao 2-1 wikiendi iliyopita na kufikisha bao la 15 kwenye Ligi Kuu England sawa na Costa ambaye aliipatia bao Chelsea ilipoishinda Hull City 2-0.

Wakali hao ndio wanaoongoza kwa ufungaji kwenye Ligi Kuu England kwa sasa.


Arsenal ina kazi ya kumbakiza Sanchez ambaye ana miezi 18 kwenye mkataba wake na anataka dau kubwa la mshahara wakati Costa katika siku za hivi karibuni amevurugwa baada ya timu za China kumpandia dau kiasi cha kugombana na kocha wake, Antonio Conte.

No comments