DIEGO SIMEONE APIGIWA NDOGONDOGO KUINOA ARSENAL

MWANASOKA wa zamani, Stan Collymore ameonya Arsenal isahau suala la kushinda vikombe ikiwa chini ya Arsene Wenger na badala yake imwajiri Diego Simeone.

Someone kwa sasa anainoa Atletico Madrid na ameifanya kuwa timu tishio Hispania na Ulaya.

Collymore ametoa kauli hiyo baada ya Mesut Ozil kutoa sharti la kubakia katika klabu hiyo la kuhakikisha kama Wenger atabaki msimu ujao.

“Ozil hayuko sahihi, yeye nadhani angetoa sharti la kuwa anataka kuiona klabu ikitengeneza timu ya kupigania vikombe kwani Wenger ameshindwa katika hilo,” alisema Collymore ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa na England.


Collymore ameshauri Arsenal imchukue Simeone kwani ataleta kikosini wachezaji wenye ari ya kupigania vikombe.

No comments