DRAKE AFUTA SHOO YA J-LO ILI WAKAJIRUSHE KWA RAHA ZAO

JENNIFER Lopez alifuta onyesho lake la siku ya mkesha wa mwaka mpya mjini Miami akitaja sababu kuwa ni “kujipa muda binafsi na kukaa wa familia” na hilo lilimaanisha kupata muda zaidi wa kujiachia na mpenziwe mpya, Drake.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 47, alionekana katika onyesho la rapa huyo la mkesha wa mwaka mpya katika klabu ya usiku ya Hakkasan, Las Vegas akimshangilia wakati akiwa amekaa katika siti ya VIP.

Alikaa katika meza maalum ya rapa huyo kwa mujibu wa video iliyopostiwa kwenye Twitter Charney Amhara wa Fox-5.

E!News iliripoti kwamba ilikuwa ngumu kumtambua Lopez katika onyesho hilo akiwa amevalia gauni jeusi na alikuwa ametulia katika eneo la VIP na rafiki zake nyuma ya jukwaa la Dj.

Kisha wawili hao wakaondoka pamoja kupitia mlango wa nyuma wa klabu hiyo majira ya saa nane usiku, kwa mujibu wa E!News.


Uhusiano wa J-Lo na Drake, 30, umezua mijadara kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakizungumzia tofauti ya umri kati yao.

No comments