DULLY SYKES ATABIRI KUENDELEA KWA BIFU LA DIAMOND, KIBA HADI BAADA YA MIAKA MITANO

MKONGWE wa muziki wa Kizazi Kipya, Dully Sykes ametabiri kuendelea kwa uhasama kati ya Ali Kiba na Diamond Platnumz kwa madai kuwa kuna watu wengi wanaosababisha ugomvi wa wawili hao wanaokubalika zaidi nchini kwa sasa.

“Katika mazingira haya ni ngumu kuwapatanisha kwa sasa kwani nyuma yao kuna watu wengi wanaoshabikia, hivyo ninadhani bado kuna miaka kadhaa kufikia tamati kwa ugomvi huo,” alisema Dully.

Alisema anatamani kuwapatanisha wasanii wenzake hao lakini sio kwa sasa hadi baada ya miaka mitano ambayo anaamini kwamba utakuwa ni wakati mwafaka kwake kufanya hivyo.


Dully alisema kuwa ana uwezo wa kuwapatanisha wasanii hao lakini hadi muda utakapofika.

No comments