ERIC BAILLY AWAAMBIA REAL MADRID "WAMWACHE KIDOGO" NA UNITED YAKE


MLINZI wa kati wa Manchester United, Eric Bailly amewaambia Real Madrid kuachana na azma ya kutaka kumng'oa kwa sababu haoni sababu ya kutaka kuachana na timu yake ya sasa licha ya klabu hiyo ya Hispania kuvutiwa naye.

Kwa msisitizo Eric Bailly amesisitiza kuwa anajisikia furaha na maisha ndani ya klabu yake ya sasa ndani ya viunga vya Old Trafford.

Kauli ya Bailly inakuja siku chache baada ya kuwepo kwa uvumi kuwa vinara hao wa La Liga wanataka kumng'oa Old Trafford kwa mapendekezo ya kocha Zinedine Zidane.

“Taaliza hizi za klabu nyingi kunihitaji zinanipa faraja na heshima kubwa lakini dhamira yangu ya sasa ni kuendelea kubaki hapa kwani bado nina kandarasi ndefu kuendelea kuweko United” alisisitiza.

Kwa sasa beki huyo mwenye umri wa miaka 22 anatajwa katika dili la usajili Real Madrid.


Raia huyo wa Ivory Coast alithibitisha taarifa za kutakiwa na wakongwe hao lakini akakanusha kuhusu kukubali kujiunga nao katika majira ya kiangazi.

No comments