FID Q AMVULIA KOFIA NAY WA MITEGO... sasa yuko tayari kupiga nae kolabo

WIMBO “Sijiwezi” wa Nay wa Mitego umemkuna vilivyo rapa mkongwe Fid Q na sasa amesema kuwa yuko tayari kufanya kolabo na msanii huyo machachari asiyeishiwa vituko.

“Kwa kweli wimbo huo umekaa vizuri, hasa ile chorus, niko tayari kufanya nae kolabo kwani nimeufatilia sana muziki wa Nay wa Mitego na kugundua kuwa yuko vizuri,” alisema Fid Q.

Rapa huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa “Kemosabe” alisema kuwa Nay sio rapa mwepesi kama ambavyo mwenyewe amekuwa akijiona bali ni miongoni mwa marapa wenye uwezo mkubwa.


Hata hivyo kwa upande wake, Nay wa Mitego alisisitiza kuwa hawezi kujilinganisha na Fid Q kwa madai kuwa yeye (Nay wa Mitego) bado ni rapa mwepeasi.

No comments