FIFA YAKUBALI KULIFANYA KOMBE LA DUNIA KUWA NA TIMU 48 KUTOKA TIMU 32

KATIKA kikao kilichofanyika Zurich, Uswisi, FIFA imekubali kuifanya michuano hiyo kuwa na timu 48 kutoka 32 za sasa na utekelezaji wake utaanza fainali za mwaka 2026.

Mabadiliko hayo ni ya kwanza kufanyika kwenye michuano hiyo tangu mwaka 1998.

Kufuatia mabadiliko hayo, Afrika na Asia zitaongezewa wawakilishi na kufikia tisa wakati nchi za Ulaya zinatazamiwakuongezewa kutoka 13 hadi 16.

Uamuzi juu ya suala la mgawanyo wa uwakilishi utatangazwa mwezi Mei, mwaka huu wakati mwenyeji wa fainali za 2026 atatangazwa 2020.

Kuanzia fainali za mwaka 2026, nchi 48 zitafuzu na kugawanywa katika makundi ya timu 16 ya nchi tatutatu.

Ili kuepusha timu kupanga matokeo, FIFA inaangalia uwezekano wa kutumia mtindo wa kupigiana penati ili kila mechi iwe na mshindi.


Nchi mbili zitafuzu kwa hatua ya mtoano ambayo itashirikisha timu 32.

No comments