FIFA YAMKAANGA JOEL MATIP DHIDI YA LIVERPOOL

SHIRIKISHO la soka la Kimataifa (FIFA), limeitaka Liverpool ipime kwa kuangalia kanuni kama inaweza kumchezesha Joel Matip ambaye amegoma kucheza Cammeroon kwenye fainali za Kombe la Mataifa Afrika.

Liverpool ilimuondoa Matip kwenye kikosi chake kilichoikabili Manchester United wikiendi iliyopita kufuatia mvutano baina ya beki huyo na nchi yake ya Cameroon.

Klabu hiyo iliomba ufafanuzi FIFA kufuatia kitendo cha Matip kutangaza amestaafu soka la kimataifa pamoja na kutakiwa kikosi cha Cameroon.

Kanuni za FIFA zinaeleza kuwa mchezaji anapokataa kuchezea taifa lake kwenye mashindano ya kimataifa, basi pia hapaswi kuchezeshwa na klabu katika kipindi hicho.


Liverpool imeshikilia kuwa Matip hayumo katika orodha ya Cameroon inayoshiriki mashindano ya Gabon ingawa nchi hiyo imekataa kumuidhinisha kuendelea kuchezea klabu yake.

No comments