FILIPE LUIS AZIINGIZA VITANI, MANCHESTER UNITED NA MANCHESTER CITY

MLINZI wa kushoto wa Atletico Madrid, Filipe Luis ameziingiza vitani klabu za Manchester United na mahasimu wao, Manchester City ambao kila moja inasaka saini yake ifikapo kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi.

Filipe Luis amekuwa muhimili mkubwa wa idara ya ulinzi ya Atletico Madrid na tayari United wamekuwa wa kwanza kuingia katika mbio za kumsajili pindi litakapofunguliwa dirisha la mwezi huu ama lile la kiangazi.

Pamoja na United na City, pia beki huyo amewavutia mabingwa watetezi wa Ligi ya serie A, Juventus ambao nao walianza kufanya mazungumzo nae katika usajili wa majira ya baridi lakini dili hilo halikukamilika.

Mwanzoni mwa msimu huu Juventus walijitosa katika mbio za kuwania saini ya Luis waliporidhishwa na kiwango chake pindi timu zao zilipokutana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa mwaka jana.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya klabu ya Atletico Madrid zinathibitisha kuwa raia huyo wa Brazil ana mkataba unaofikia tamati mwaka 2018 ingawa tayari wameanza mazungumzo ya awali ya kumuongezea mkataba mpya.


Magazeti ya nchini Hispania yamethibitisha taarifa kuwa Manchester City wameshaanza mazungumzo na klabu hiyo ya La Liga huku kocha mpya, Pep Guardiola akitajwa kuwa ndie anaefanya mpango kumnyakua mlinzi huyo.

No comments