GHANA WAONYESHA KUWA NA "USONGO" NA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

GHANA wataingia na jambo moja tu kuhakikisha wanatwaa Kombe la Mataifa Afrika zinazofanyika nchini Gabon, mwaka huu.

Ina kila sababu ya kujiamini kutokana na kuwa na kikosi kinachoundwa na wachezaji wazoefu katika fainali hizo.

Nyota hao ni pamoja na nahodha Asamoah Gyan ambaye amecheza mara sita kwenye mashindano hayo na kufika fainali mara mbili ambapo mara zote walishindwa.

Pia kikosi hicho kinajivunia ndugu wawili Andre na Jordan Ayew ambao ni watoto wa mwanasoka nyota wa zamani wa Ghana, Abedi Pele na tegemeo katika kikosi hicho.


Pamoja na yote, wana kocha mzoefu raia wa Israel, Avram Grant ambaye amekuwa na kikosi hicho tangu mwaka 2014.

No comments