RAPA wa siku nyingi, King Crazy GK amesema kuwa njia pekee ya kuwafanya wasanii kujiepusha na mambo ya kuwaharibia maisha ni kurudi shuleni ili wapate elimu itakayowawezesha kufanya kazi nyingine pale muziki utakapogoma.

Amesema, hata wale wanaojiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya wanachanganyikiwa katika maisha wanapokwama kwenye muziki wakidhani kuwa zitawasaidia kumbe wanajiharibia.

“Wasanii wengi huingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya kutokana na kutegemea muziki peke yake na pale wanapochuja huchanganyikiwa na kutafuta kujiliwaza kwa “unga” na kumbe wanazidi kuharibikiwa,” amesema GK.


Amesema kuwa, kuna haja serikali kuwachukulia hatua kali watu wanaosambaza dawa hizo ili kukomesha kuwepo kwa dawa hizo hapa nchini kwa vile zinachangia kuharibu vijana wengi.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac