H MBIZO AVAMIA JUKWAA LA JAHAZI MODERN TAARAB NA KUPAGAWISHA MASHABIKI KWA NGOMA CHINI ZA “KUTUNGA”

MKALI wa Bongofleva, Hamis Mbizo “H Mbizo” Alhamisi iliyopita aliushangaza umati wa mashabiki baada ya kukamata kipaza sauti kwenye shoo ya Jahazi Modern Taarab na kurindima kwa kuimba vipande vya vionjo kutoka klichwani kwake akifuatisha sebene la wimbo “Full Shangwe”.

Tukio hilo la aina yake na lililovuta hisia za wengi lilitokea kwenye ukumbi wa mavuva, Magomeni Makuti ambako Jahazi Modern ilikuwa ikitumbuiza siku hiyo.


Prince Amigo ndiye aliyemkaribisha jukwaani H Mbizo na kumwomba awape mashabiki wa taarab ladha ya vionjo kutoka kichwani kwake, ndipo mkali huyo alipoanza kutiririka “ngoma chini” ambazo inaonekana alizitunga papo kwa hapo lakini zilionekana kuwapagawisha wengi.

No comments