HASSAN BITCHUKA ATOA KALI YA MWAKA... asema anajiona bado hajui kuimba

MKONGWE wa uimbaji kutoka ndani ya Sikinde Ngoma ya Ukae, Hassan Bitchuka hivi karibuni ametoa kali alisema kuwa anajiona bado hajui kuimba.

Katika mazungumzo yake na Saluti5, Bitchuka amesema kwamba anashaa kuona watu wanampa sifa nyingi utasema amefika mwisho wa ufundi wa uimbaji wakati kumbe muziki hauna kikomo kama ilivyo katika suala la elimu.


“Nacheka sana watu wanaposema kuwa eti Bichuka anajua kuimba… mimi bado sijajua bwana na hata hao wengine wanaojiona kuwa wanaweza nao bado vilevile,” alisema nguli huyo mwenye sauti inayoweza kumtoa nyoka pangoni.

No comments