Habari

HATIMAYE MANCHESTER UNITED YAKUBALI KUMPIGA BEI MEMPHIS DEPAY KWA LYON YA UFARANSA

on

Manchester United imekubali kumuuza winga Memphis Depay kwenda Lyon ya Ufaransa kwa dau litakalofikia pauni milioni 21.6. 
Kimsingi vilabu hivyo viwili vimekubaliana ada ya pauni milioni 16 ambayo itaongezeka baadae hadi pauni milioni 21.6 kutegemeana na mafanikio itakayoyavuna Lyon.
Depay alijiunga na United kutoka PSV Eindhoven kwa ada ya pauni milioni 25, ambayo inaonyesha kuwa klabu hiyo ya Old Trafford itapata hasara kidogo kwa mauzo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliyekuwa akilipwa pauni 100,000 kwa wiki.
Depay atafanya vipimo vya afya kabla ya wikiendi na tayari ameshakubali mkataba wa miaka minne na nusu kwa miamba hiyo ya Ufaransa. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *