IAN WRIGHT AMTABIRIA MOUSA DEMBELE KUIUA CHELSEA USIKU HUU

STRAIKA wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amemtaja kiungo wa Tottenham Hotspur, Mousa Dembele kuwa ndiye atakayeiua Chelsea leo.

Tottenham inaikaribisha Chelsea kwenye mechi ya Ligi Kuu England itakayopigwa kwenye uwanja wa White Hart Lane.

“Dembele ndio silaha muhimu ya Tottenham kuiua Chelsea kwenye mechi baina yao,” alisema Wright ambaye ni mchambuzi wa soka.

Chelsea imeshinda mechi 13 mfululizo kwenye Ligi Kuu na ikishinda leo itaifikia rekodi ya Arsenal ya kushinda mechi 14 mfululizo.


Wright alisema umahiri wa Dembele kwenye kiungo ndio utaisambaratisha Chelsea ambayo imekuwa haizuiliki.

No comments