IBRAHIMOVIC AMCHANA MARTIAL "DOGO ACHANA NA WAPAMBE, MZINGATIE MOURINHO TU"

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amemtaka Anthony Martial kumsikiliza kocha Jose Mourinho na sio wapambe.

Martial amekuwa akilaumiwa na Mourinho kwa kushindwa kuonyesha kiwango pale anapopangwa.

Kufuatia hali hiyo ya kutoelewana baina ya watu hao wawili, inadaiwa wakala Phillipe Lamboley alikuwa anasuka mipango ya martial kwenda kucheza Sevilla kwa mkopo.


“Nimempa ushauri Martial amsikilize Mourinho na aache kusikiliza watu wa pembeni,” alisema Ibrahimovic.

No comments