Habari

IBRAHIMOVIC ASEMA ATAENDELEA KUWAFUNGA MIDOMO WANAOMKOSOA

on

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic  amesema amewafunga mdomo wachambuzi wa soko waliokuwa na mashaka juu ya uwezo wake wa kusakata soka la hali ya juu katika umri wa miaka 35 alionao.

Ibrahimovic alihitaji goli moja tu kufikia rekodi ya mabao 51 aliyofunga Lionel Messi kwa mwaka 2016, lakini Msweeden huyo anasema haihitaji rekodi hiyo ili kuwaumbua waliokuwa wakisema amekwisha kisoka wakati akitua Old Trafford.

“Najisikia niko vizuri,” anaeleza Ibrahimovic. Sijui nimebakiza miaka mingapi ya kucheza soka, lakini nafurahia soka langu.

“Nilikuja kwenye Premier League huku kila mtu akiamini kuwa itakuwa ngumu kwangu, lakini siku zote nimefanikiwa kuwafanya watu wameze maneno yao.

“Inanipa nguvu nyingi kwasababu wao wanalipwa kwa maongezi yao na mimi nalipwa kwa kucheza na miguu yangu. Hivi ndiyo ninavyofurahia soka langu.

“Kila mwaka vilabu vya Premier League vilikuwa vikihitaji huduma yangu lakini sikushawishika, nilitaka kuja hapa wakati kila mtu akiamini kuwa nimekwisha”.

Ibrahimovic ameifungia United magoli 17 yakiwemo 12 ya Premier League. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *