IRENE PAUL AIPIGIA DEBE TAMTHILIA YA "HUBA"

MKALI wa Bongomuvi, Irene Paul ameisifu tamthilia anayoshiriki ya “Huba” akisema imeleta mapinduzi katika sanaa ya maigizo nchini na kwamba msimu wake wa pili unaoanza mwaka huu mpya wa 2017 utakuwa ni balaa zaidi.

Tamthilia hiyo kali inayowashirikisha nyota kadhaa wakiwemo Riyama ally, Muhogo Mchungu, Mboto, Rammy Galis, Grace Mapunda na Kidoa Salum inarushwa mara mbili kwa wiki na channel ya DSTV ya Africa Magic Bongo.

Alisema kuwa kwa sasa sehemu ya kwanza ya tamthilia hiyo imekuwa ikirushwa hewani huku yeye na wenzake wakiendelea kuandaa sehemu nyingine ikiwemo ya pili itakayoana kurushwa Februari.


Irene amewataka mashabiki wa tamthilia kuifuatilia “Huba” akisema ina hadithi adimu sana iliyojaa kila aina ya mkasa wa mapenzi, migongano ya kifamilia na visa vya chuki katika jamii.

No comments