Habari

IVORY COAST IKIWA NA MASTAA KIBAO YAVULIWA UBINGWA NA MOROCCO …Eric Bailly ‘apeleka’ neema Manchester United

on

Ivory Coast ikiwa na wachezaji wake wazoefu na wenye majina makubwa, imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kulambwa 1-0 na Morocco katika hatua ya makundi.
Dakika ya 64 Rachid Alioui akiwa nje ya box akamchungulia kipa Gbohouo na kuachia shuti la juu lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Ivory Coast inatolewa baada ya kujikusanyika pointi mbili huku Morocco na DR Congo zikisonga mbele katika kundi C.
DR Congo imeongoza kundi C baada ya kuinyuka Togo 3-1 na na kufikisha pointi 7 wakati Morocco ikifikisha pointi 6 huku Togo ikishika mkia kwa kuambulia pointi moja.
Kutolewa kwa Ivory Coast kunaweza kuwa ni habari njema kwa kocha wa Manchester United Jose Mourinho ambaye sasa ataungana tena na beki Eric Bailly.
Morocco (3-4-3): Mohand; Benatia, Da Costa, Saiss; Dirar, El Ahmadi, Boussoufa, Mendyl; Fajr (Obbadi 82); Bouhaddouz (Alioui 42, Boutaib 92), En-Nesyri 
Ivory Coast (4-3-3): Gbohouo; Aurier, Bailly, Deli, Kanon; Doukoure (Seri 52), Die, Kessie (Gradel 84); Zaha (Kodjia 75), Bony, Kalou.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *