IVORY COAST YAANZA KWA MBINDE FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA

VOGOGO vya soka barani Afrika, Ivory Coast wamejikuta kwenye wakati mgumu kwenye fainali za Kombe la Mataifa zilizoanza wikiendi iliyopita nchini Gabon.

Ivory Coast ilijikuta ikilazimishwa suluhu na Togo Jumatatu wakati Morocco ikilala kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mechi nne kati ya sita za mwanzo zimemalizika kwa sare, ambapo Cameroon walifungana na Burkinafasso bao 1-1, wakati Algeria ilifungana mabao 2-2 na Zimbabwe.

Pia wenyeji Gabon walitoka sare ya bao 1-1 na Guenea Bissau wakati Senegal iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tunisia.


Katika mechi ya kwanza Jumatatu, Togo ilionekana kuwa fiti zaidi wakati wakiongozwa na staa wao, Immanuel Adebayor wakati Morocco ilicheza kitimu zaidi pamoja na kulala kwa Congo.

No comments