J-LO AMFICHA DRAKE KWA FAMILIA YAKE NA WATU WAKE WA KARIBU

NYOTA wa filamu na muziki, Jennifer Lopez anataka mahusiano yake na rapa Drake yawe “mepesi, yasiyo na presha na yenye furaha” ndio maana hajaifahamisha familia yake.

Mwanamama huyo aliyeolewa mara tatu anatajwa kukosa bahati katika mapenzi na hataki yaliyopita yajirudie tena na hataki kuingia mzimamzima haraka katika mahusiano na Drake, 30, anayetoka nae sasa.

Chanzo kiliiambia Hollywoodlife.com: “Hayazungumzii mahusiano yake mapya kwa rafikize na familia na badala yake anajaribu kufanya mambo taratibu. Anataka kuona mambo yanaenda ngazi kwa ngazi, kiuwepesi na furaha.”

“Anajua kwamba drake ni kijana mwenye tabia ya kupenda kuwa na wanawake wengi kidogo, hivyo ili kuepusha kuharibu anajaribu kupeleka mambo hatua kwa hatua bila ya kuweka presha kwa Drake.”


“Jambo ambalo Jennifer anaogopa kabisa lisitokee ni kuonekana mjinga ama amechezewa tu na Drake.”

No comments