JACKLINE WOLPER AWATAKA WASANII KUJIPANGA KUIRUDISHA BONGOMUVI KWENYE CHATI

MWIGIZAJI wa filamu, Jackline Wolper amesema kuwa iko haja kwa wasanii wa fani hiyo kujipanga upya ili kubaini ni wapi walipokosea kwa lengo la kuirudisha Bongomuvi kwenye hadhi yake.

“Kwa mtazamo wangu ni kwamba Bongomuvi haijafa kama ambavyo baadhi ya watu walivyokuwa wakidai bali inapitia kwenye changamoto tu, hivyo ni vyema wasanii tukae tutafakari ni wapi tulikosea ili tuirudishe kwenye chati,” alisema Wolper

Alisema kwa muda mrefu amejikita zaidi kwenye biashara zake na kufafanua kuwa hatua hiyo haimaanishi kwamba Bongomuvi imekufa bali ameamua kujiongezea kipato kwa njia ya biashara.


“Niendelee kuwatia moyo wasanii wenzangu kuwa Bongomuvi haijafa, tujipange upya kwa kuangalia mapungufu na kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo, hili litawezekana kwa kuimarisha umoja wetu,” alisema.

No comments