JAHAZI MODERN TAARAB YAWAOMBA RADHI MASHABIKI WAO WA BUGURUNI


BENDI ya Jahazi Modern Modern Taarab imewaomba radhi mashabiki wao wa Buguruni kutokana na tukio la Jumapili ndani ya Lekam Royal Hotel la kukatiza shoo kabla ya muda wake na kuwaahidi kutojitokeza tena.

Hamis Boha ambaye ni mmoja wa mabosi wa bendi hiyo inayokusanya waimbaji nyota kama vile Prince Amigo, Mwasiti Kitoronto, Mosi Suleiman, Zubeda Mlamali na Fatma Kassim, amefunguka kuwa waliangushwa na suala la kukosa kibali cha muda.

“Tumesikitika sana kwa tukio hilo lakini tunawaomba radhi mashabiki wetu na kuwaahidi kutojitokeza tena kwa wiki zijazo kwani hivi sasa tumelifungia kazi kuhakikisha tunapata mwafaka wake,” amesema Boha.

Amesema kuwa, wiki hii wataendelea kupiga katika ukumbi wao huo wa nyumbani na wanaamini hakutakuwa na kizingiti chochote kitakachowafanya wakatize shoo na kumaliza kabla ya muda unaojulikana.

No comments