JAMIE CARRAGHER AZITAKA MANCHESTER UNITED, CITY KUSAHAU UBINGWA MSIMU HUU

BEKI wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher amesema kuwa Manchester United na Manchester City zisahau suala la kutwaa ubingwa.

Manchester United ilitoka sare ya 1-1 na Liverpool waka Manchester ikichakazwa mabao 4-0 na Everton wikiendi iliyopita.

Matokeo hayo yamezifanya Manchester City na Manchester United kuwa pointi 10 na 12 nyuma ya Chelsea inayoongoza Ligi Kuu England.

“Manchester City na United zimeachwa nyuma sana kwenye msimamo, sidhani kama zina nafasi tena.” Aliongeza Carragher.


Carragher alisema Chelsea, Tottenham Hotspur, Liverpool na Arsenal ndizo zina nafasi ya kutwaa ubingwa.

No comments