JAQUELINE WOLPER: HABARI ZA KUACHANA NA HARMONIZE NIACHIENI MWENYEWE

NYOTA wa filamu Bongo, Jaqueline Wolper ameomba abebe mwenyewe sakata linaloendelea sasa la kuwepo kwa habari za kuachana na mpenzi wake msanii wa Kizazi Kipya, Harmonize.

Wolper amesema kuwa kwa sasa hataki kuliweka wazi jambo hilo na kwamba likimshinda atashirikisha watu wengine na kwamba kuna baadhi ya mambo yanayoendelea ambayo anayachukulia kama sanaa tu.

“Naombeni niendelee nalo mwenyewe kwanza nikiweza nitaliweza au vinginevyo nitawashirikisha, hayo mengine mnayosikia ni sanaa tu na “kiki” ambazo watu wanazitengenezea habari,” alisema Wolper.

Msanii huyo amesema amekuwa akipokea simu za watu wengi na wengine kumfuata dukani kwake kumuuliza kama wanayoyasikia ni ya kweli ama uzushi, lakini anawajibu kwamba hana la kusema.


Pamoja na maelezo hayo, Wolper aligusia kidogo bila kutoa ufafanuzi kwa kusema kwamba tangu angali mdogo anapenda mapenzi na anaheshimu sana mahusiano.

No comments