JAY MOE APONDA ZOEZI LA KUWACHANGIA FEDHA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA

RAPA mkongwe, Jay Moe amesema haoni umuhimu wa kuwachangia fedha wasanii waathirika wa dawa za kulevya kwa madai kwamba hatua hiyo inaweza kusababisha wengine zaidi kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo wakijua watachangiwa fedha.

Alisema kuwa wasanii wote ambao ni waathirika wa dawa hizo wanatawaliwa na ushamba wa kupenda kuiga mambo ambayo hawana uwezo nayo na mwisho wake wanajikuta wakiwa katika hali hiyo.

“Mimi sioni sababu yoyote ya kufanya tamasha na kuchangia fedha watu washamba kama hao wanaopenda kuiga mambo wasio na uwezo nayo,” alisema Jay Moe.


Alisema, wasanii wan je wanaotumia dawa hizo wana pesa nyingi na wana uwezo wa kubadilisha damu lakini ajabu hata wasanii wasio na pesa wa Tanzania nao bila kujua hilo wanajiingiza katika matumizi hayo.

No comments