JB AWASHUKIA WAANDAAJI MUVI WAKWARE... awataka wabadilike

MKONGWE wa Bongomuvi, Jacob Stephen “JB” amesema kuwa watayarishaji wanaowaingiza waigizaji kwenye filamu zao kwa ajili ya rushwa ya ngono ni wajinga na kwamba kama wapo basi wabadilike.

“Kwa mtazamo wangu ni kwamba ni mtayarishaji mjinga ambaye atakubali kumuingiza mwigizaji kwenye filamu yake kwa ajili ya rushwa ya ngono huku akijua wazi kuwa hana uwezo wa kuigiza,” alisema JB.

Alisema kuwa kwa mazingira hayo muhusika atakuwa ameiharibu kazi yake hiyo kwa sababu haitakuwa nzuri kwavile ameweka watu wasiokuwa na uwezo.

“Mimi tangu nianze kazi hii mwaka 2003 nishatoa filamu zaidi ya 40 lakini sijawahi kupata matatizo ya soko katika kazi zangu, hivyo katika hili lazima niwe mkweli sijawahi kupata matatizo. Kazi zangu zimekuwa zikiuzwa na nimekuwa ninapata mauzo mazuri tu, hivyo hilo lazima nimshukuru Mungu.”


Alisisitiza kuwa hilo limechangiwa na kawaida ya kutumia waigizaji wenye vipaji tu.

No comments