JINI KABULA: SIJABAHATISHA KUMWIMBIA BWANA, NIMEDHAMIRIA KUOKOKA

NYOTA wa filamu, Miriam Jorwa ambaye sasa ameamua kuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili, amesema hakubahatisha katika uamuzi huo bali amedhamiria kumwimbia Mungu.

“Tangu nikiwa mdogo ninapenda kuimba kanisani, baadae mambo ya dunia yakanifanya niache lakini Mungu ameamua kuniita nimtumikie na sasa ninaandaa albamu,” alisema msanii huyo.

Msanii huyo amesema kuwa, katika maisha yake amefanya mambo ambayo sasa ameona ni bora aachane nayo kwa madai kwamba yalisababisha hadhi yake ishuke ndani ya jamii.


“Nilifikia wakati nikawa mlevi sana hadi thamani yangu ya umaarufu ikashuka lakini sasa namshukuru Mungu kwani watu wazima waliniweka chini wakanielewesha na nikaachana na ulevi,” alisema.

No comments