JOHN TERRY ASEMA ANAENDELEA KUJIPANGA UPYA KWA AJILI YA MAISHA MENGINE

BEKI mkongwe wa Chelsea, John Terry amesema anaendelea kujipanga upya kwa ajili ya maisha mengine ya soka.

“Katika soka kuna mambo lazima uyakubali, hasa katika suala la umri na maslahi ya klabu. Kinachohitajika ni tija na mafanikio,” alisema Terry.

Terry ambaye ni kama anazeekea Stanford Bridge, amekuwa akipewa mkataba wa mwaka mmoja mmoja misimu miwili iliyopita, hali inayotafsiriwa kuwa huenda siku za kubakia darajani zimeanza kuhesabika.

Hata hivyo, Terry mwenyewe amewahi kunukuliwa katika siku za hivi karibuni akieleza mpango wake wa kutaka kutimkia kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Marekani kwa kufuata nyayo za Steven Gerrard na Frank Lampard.


Awali Chelsea wamekuwa wakimmwagia sifa Terry kwa kusema ana umuhimu mkubwa ndani ya kikosi kinachopambana kwa ajili ya kulinda hadhi, ingawa tayari imeshatema taji la primier.

No comments