JONAS MKUDE ASEMA MECHI YA SIMBA NA YANGA SIO YA KUICHUKULIA POA


NAHODHA  wa klabu ya Simba Jonas Mkude, amesema mechi yao  dhidi ya Yanga sio ya kuichukulia poa kwani klabu zote mbili zina wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu.

Mechi hiyo ya Simba na Yanga inapigwa leo usiku katika uwanja wa Amani, Zanzibar ikiwa ni nusu fainali ya pili ya Kombe la Mapinduzi.

Mkude amesema mpira ni mchezo wa makosa na klabu itakayokosea ndio itakayoadhibiwa hivyo mashabiki wa klabu zote mbili wasiuchukulie kijuujuu mchezo huo.

Yanga inakutana Simba huku ikiwa na majeraha ya kulambwa 4-0 na Azam FC katika hatua ya makundi, hali inayofanya masabiki wa Simba kuamini kuwa wana mechi nyepesi usoni mwao dhidi ya watani wao hao.

Pamoja na imani hiyo ya mashabiki wa Simba lakini nahodha wa klabu hiyo ya msimbazi anatahadharisha kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwa pande zote mbili.

No comments