JONAS MKUDE AUSHUKIA MTANDAO WA GOAL KWA MADAI YA UPOTOSHAJI KUHUSU SIMBA SC

NAHODHA wa Wekundu wa Msimbazi, Jonas Mkude ameushukia mtandao wa Goal kwa madai ya kutoa taarifa za upotoshaji kuwa wachezaji wa Simba SC wanadai mishahara ya miezi miwili.

Akiongea na Saluti5 saa chache zilizopita, Mkude amesema kuwa taarifa hizo ni za uongo mkubwa na ni zenye lengo baya la kuwaondoa katika nia ya kuipa ubingwa timu yao.

“Mimi naamini mwandishi wa makala hii anatumika na wapinzani wetu. Timu inayoongoza Ligi na iliyofuzu kwenye raundi nyingine utasemaje inafanya vibaya?” alihoji Mkude.


Mkude amewaomba Wana Simba waendelee kushikamana ili kufanikisha malengo yao, huku akisisitiza kuwa mwandishi wa makala ya Goal ni mnafiki na anafaa kupuuzwa.

No comments