JOSE MOURINHO ATUPA DONGO LIVERPOOL… asema Manchester United ndio klabu kubwa England

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amejigamba kuwa klabu yake ndio kubwa England.

“Sijui klabu nyingine kubwa England zaidi ya Manchester United,” alisema Mourinho wakati akizungumzia mechi kati yao na Liverpool inayopigwa leo kwenye uwanja wa Old Trafford.

Mourinho alisema kuwa anaelewa upinzani wa jadi baina ya timu hizo mbili lakini akashikilia kuwa likija suala la timu kubwa basi ni Manchester United.


Nae kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ameonya timu yake iko tayari kuikabili Manchester United ambayo katika siku za karibuni wamepandisha kiwango chake.

No comments