JULIO ATENGUA UAMUZI WAKE WA KUSTAAFU KUFUNDISHA MPIRA WA MIGUU

BAADA ya kuamua kukaa nje ya soka kwa kipindi cha miezi miwili sasa, kocha wa zamani wa Mwadui FC na Simba, Jahamhuri Kihwelo “Julio” amesema kuwa si kwamba ameachana na mpira kabisa bali yupo njiani kurudi.

Kocha huyo mwenye maneno mengi amesema kuwa kitakachomrudisha uwanjani ni mabadiliko ndani ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi Tanzania.

Julio alisema: “Niliamua kuachana na mpira kutokana na kasoro ambazo ziko kwa TFF, si kwamba nilizuiwa na kusimamishwa.”

“Nataka niseme hivi, nitarudi siku TFF na Bodi ya Ligi itakaporekebisha mambo fulani ambayo yalikuwa yakiathiri utendaji wake kwenye mashindano ya Ligi Kuu.”

“Nafahamu kuwa wanasema mengi lakini nitawaambia tu siku ambayo nitarudi kwa kuwa nina nia ya kuendelea kufundisha na kushindana.”


Hapo awali kabla ya kujiuzulu kuifundisha Mwadui, kocha huyo tayari alikuwa akilalamikia maamuzi ya waamuzi kwenye kila mechi ambayo alikuwa akicheza akiwatuhumu kupendelea timu nyingine na TFF kulinyamazia hilo.

No comments