JUVENTUS YAMWINDA STRAIKA ANDRE AYEW WA WEST HAM UNITED

STRAIKA Andre Ayew anawindwa na kibibi kizee cha Turin, Juventus ingawa kutakuwa na kazi ya ziada kumng’oa katika timu yake ya sasa ya Westham United.

Juve imekuwa katika mbio za kumsainisha nyota huyo kwa dau la pauni mil 27.

Hatua ya Juventus kutaka kumwita kundini mtoto huyo wa mfalme wa zamani wa soka barani afrika, Abed Pele ni kutokana na mkakati wake wa kutaka kukisuka kikosi bora katika Ligi ya serie A kwa mafanikio makubwa msimu ujao.

“Ayew ni kati ya wachezaji muhimu kwa sasa ulimwenguni, ana kipaji cha kuweza kucheza katika klabu yoyote kubwa, hivyo Juve haipaswi kumwacha.”

“Ana sifa moja kubwa nayo ni kuweza kubadilisha mchezo wakati wowote, anajua kufumania nyavu wakati wowote hata katika mazingira magumu.”


“Kizuri ambacho ni sifa yake ya ziada ni kwamba ni mzuri katika kupiga pasi za mwisho, hivyo ni straika muhimu kwa sasa katika kiwango cha soka la dunia,”kimenukuliwa chanzo cha uhakika ndani ya Juventus.

No comments