KALA JEREMIAH AMPONDA DARASA NA WIMBO WAKE WA "MUZIKI"... asema hauna ujumbe wowote

RAPA Kala Jeremiah amedai kuwa wimbo wa rapa mwenzake, Darasa uitwao “Muziki” hauna ujumbe wowote ila watu wametokea kuupenda tu bila kuambulia chochote wanachoweza kubakia nacho kichwani.

“Kwanza nikiri kwamba mimi ni shabiki mkubwa wa wimbo huo, lakini ukweli utabaki palepale tu kuwa “Muziki” hauna ujumbe wowote, hata Darasa mwenyewe analijua hilo kwa sababu sio siri,” alisema Kala.

Kala aliongeza kwa kusema: “Ninaposema hauna ujumbe maana yangu ni kwamba watu wanausikiliza na ukishamalizika hakuna wanachobaki nacho kichwani, ni tofauti na ule wa kwangu wa “Wana Ndoto”.”


Alisema kuwa yeye ni miongoni mwa wale wanaoshabikia wimbo huo lakini akiulizwa ni kwa sababu gani hawezi kuelezea na pia amekuwa akiutumia kumbembelezea mwanawe anapolia kwavile nae anaupenda.

No comments